April 14, 2020


UONGOZI wa Simba umesema kuwa kwa sasa unaiachia Serikali ishu ya wachezaji wao kurudi Bongo kutokana na wao kutokuwa na namna ya kufanya.

Nyota wa Simba ambao ni Meddie Kagere, Francis Kahata na Sharaf Shiboub wapo nje ya nchi na mipaka kwao imefungwa kutokana na kujilinda na maambukizi ya Virusi vya Corona.

Kagere yupo Rwanda, Kahata yupo Kenya na Shiboub yupo Sudan wakiwa nje kwa mapumziko baada ya Serikali ya Tanzania kusimamisha shughuli zote zinazhusu mijumuiko isiyo ya lazima.

Akizungumza na Saleh Jembe, Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema kuwa hawana cha kufanya kwa nyota hao kuweza kurejea nchini kwa sasa.

"Hakuna namna ambayo tunaweza kuifanya kwani Serikali imefunga mipaka hivyo kuhusu kurudi kwao ni juu ya Serikali na itategemea kutengamaa kwa hali ya maambukizi, ila kwa sasa hatuna cha kusema," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic