April 14, 2020



GOLIKIPA wa zamani wa timu ya taifa, Taifa Stars, Ivo Mapunda, amemshauri kipa wa Simba, Beno Kakolanya kwenda kutafuta changamoto nje ya nchi ili kulinda kipaji chake alichonacho cha kuokoa michomo golini. 

Kakolanya alijiunga na Simba kwenye msimu huu wa Ligi Kuu Bara akitokea Yanga baada ya mkataba wake wa miaka miwili ya kuichezea timu hiyo kumalizika. 

Kipa huyo tangu ametua kujiunga na Simba, amekuwa hapati nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo huku akimuachia Aishi Manula ambaye ndio pendekezo la kwanza la Mbelgiji, Sven Vandenbroeck. -

 Mapunda amesema kuwa Kakolanya ni kati ya makipa bora nchini ambaye anaamini kama akitoka kwenda kucheza nje ya nchi, thamani yake itaongezeka tofauti na ilivyo hivi sasa.

2 COMMENTS:

  1. Sipendelei kujadili masuala ya wanasoka kwenda kutafuta maisha au changamoto nje ya nchi yetu.Ushauri kama aliotoa Ivo Mapunda kwangu shauri lake hauna mantiki.Kinachopewa kipaumbele na muhimu ni maslahi Kwa ajili ya maisha yako ya sasa na baadaye.Kakolanya amecheza mechi za kutosha hadi sasa pale Simba wakipokezana na Manula.Unamwambia akatafute changamoto nje ya nchi kwani huko una uhakika kuwa atapata masilahi mazuri zaidi ya alipo Kwa sasa? Muhimu ktk maisha ya mchezaji wa soka ni masilahi na umri ndio vya kuzingatia.Nakumbuka miaka ya mwishoni ya 60 Yanga ilikuwa na makipa wawili Elias Michael na Muhidin Fadhil na wote wenye uwezo uliofanana na walikuwa wanapokezana...miaka ya 70 nao Simba walikuwepo Mambosasa na Mahadhi...Yanga tena miaka ya 80 kina Kinye na Nemes...Simba tena Mwameja na Iddi Pazi na sio Simba na Yanga hata timu zingine zilikuwa na makipa wawili wenye uwezo unao fanana kama Pamba FC, Coastal Union n.k.
    Bado nashangazwa sana na wale wanao mlaumu Ajib ya kutokwenda TP Mazembe.Nilimsikia Ajib akisema ofa ya Simba ilikuwa nzuri kwake kuliko ya Mazembe hivyo ni uamuzi wake na familia yake baada ya kutafakari changamoto atakazokutana nazo mbele ya safari ya maisha take.Lazima ujue kuchanga karata zako za maisha.
    Wako wapi kina Peter Manyika,Chilunda,Kichuya, Jamal Mwambeleko,na wengineo wengi wameishia kusiko-julikana walikoenda kujaribu kucheza soka nje ya nchi tokea miaka ya 1978.Ni vizuri kuwashauri vijana wakapitia soccer academy na baada ya hapo wanatafuta biashara ya kucheza nje wakiwa na umri under 20.Vinginevyo unamshauri mchezaji ana zaidi ya umri wa 23 tena ana familia inayo mtegemea ni kujidanganya.Ivo tafakari Kwa ushauri wako Kwa Kakolanya.

    ReplyDelete
  2. Africa masharik hakuna timu unalipa vzr Kama Simba aende sbb anatafuta sifa au? na hata Tanzania hakuna labda Azam. Changamot ya namba haikimbiw unaikabili. Mi nidhan angemshaur apambane aongee akiwa mchezon amepoa Sana sk hizi sio Kama alivyokuwa yanga

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic