April 14, 2020

UONGOZI wa Simba umesema kuwa upo kwenye mpango wa kuwashtaki Yanga kutokana na suala lao la kutaka kuipata saini ya nyota wao Clataos Chama raia wa Zambia.

Yanga imeripotiwa kuwa kuanza kufanya mazungumzo na Chama ambaye ni mali ya Simba jambo ambalo ni kinyume na utaratibu wa Shirikisho la Soka Duniani (Fifa) kwa kuwa Simba inaeleza kuwa ana mkataba mrefu ndani ya Simba.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa ni lazima kanuni zifuatwe na kusimamiwa hivyo kwa kosa lao la kufanya mazungumzo na Chama watawashtaki.

"Kanuni za mpira zipo wazi na jambo ambalo linazungumzwa ni kinyume na utaratibu uliopo ni lazima tufanye jambo ili kuwafunnza Yanga katika hili, ipo wazi kabisa," amesema.

Chanzo: Wasafi

6 COMMENTS:

  1. Ndio mana ukaitwa Mzukule wa simba,Unababaika babaika babaika nini sasa wakati mnajifanyaga mna pesa,mbona umeanza uoga sasa,Wewe kweli mzukule wa Simba..

    ReplyDelete
    Replies
    1. 😂😂😂 tuliza ball.

      Delete
    2. Mnaambiwa ukweli kuwa mnakiuka sheria na wewe unatoa mipovu na matusi.Toa hoja ili ijadiliwe kama CEO alivyosema kuwa biashara inaweza ikafanyika Kwa kuweka dau la kuvunja mkataba.Viongozi wa Simba hawajatoa matusi hivyo wadau twende na wakat.

      Delete
    3. Kwenye pesa hakuna ukweli zuzu wewe

      Delete
  2. Mwakalebela kanywea. Nyoo utazungumza vipi na mchezaji mwenye mkataba mrefu?Washtakini ili iwe fundisho.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic