April 14, 2020


UONGOZI wa Simba umesema kuwa kiungo wao Clatous Chama raia wa Zambia mkataba wake bado unaishi mpaka pale Juni 2021.

Chama amekuwa akihusishwa kujiunga na wapinzani wa Simba Yanga ambao inaelezwa kuwa wameanza kufanya mazungumzo na nyota huyo ambaye kwa sasa yupo nchiniZambia.

Ofisa Habari wa Simba Haji Manara amekanusha taarifa kuhusu mkataba wa kiungo  Chama kumalizika mwaka huu, akisisitiza kuwa mkataba wa nyota huyo utamalizika mwezi Juni mwaka 2021.

"Timu yoyote itakayoanza kufanya mazungumzo na Chama itakuwa ni kinyume na utaratibu wa Shirikisho la Soka duniani (Fifa) hivyo walioanza waache mara moja.

"Tunajua kwamba ni mchezaji mzuri lakini bado ni mali ya Simba kwa sasa labda kama walikuwa hawajui bado ni mali yetu na haendi popote pale," amesema.

4 COMMENTS:

  1. Kwani mkataba wake ulikuwa miaka mitatu!? Na kama mnasema amesaini mkataba mwingine wa miaka miwili, je miaka miwili inaishia 2021 au 2022!? Manala unaongea sana halafu hujitambui! Jipange kwanza, kuwa msemaji sio kuropoka!!

    ReplyDelete
  2. WEWE ndio ngedere kweli Alisaini miaka 2 tokea 2019 na miaka miwili inaisja 2021.Ulikimbia shule. Leo Mwakalebela ameomba radhi kwa kujaribu kumsajili mchezsji mwenye mkataba. Dawa ni kuwaripoti tu ili iwe fundisho.

    ReplyDelete
  3. Enter your comment...Haaaahaaaaha,MISUKULE FC IMETAHARUKI,Safari hii tutahesjiana .

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic