April 13, 2020

BERNARD Morrison, kiungo mshambuliaji wa Yanga amebadilishiwa program na kocha wake, Luc Eymael ambapo kwa sasa anafanya mazoezi ufukweni.

Morrison aliwafunga Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Machi 8, Uwanja wa Taifa.

Awali Morrison alikuwa akifanya mazoezi nyumbani tu katika kipindi hiki cha ligi kusimama kutokana na uwepo wa Virusi vya Corona, ambapo benchi la ufundi la Yanga liliwapa wachezaji wake wote program za kufanya wakiwa nyumbani.

Morrison amesema: “Awali baada tu ya ligi kusimama, nililazimika kununua vifaa vyangu binafsi vya mazoezi na nikawa ninafanya mazoezi ya asubuhi na jioni nikiwa nyumbani.

 "Kwa sasa hivi kocha kaniongezea mazoezi kwa kunitaka nihakikishe napata kipindi kimoja cha asubuhi au jioni cha kufanya mazoezi ufukweni,".

4 COMMENTS:

  1. Mwandishi alikuwa ansumia sana rohoni siku mbili hizi hajatoa taarifa ya kipenzi chake

    ReplyDelete
  2. Mwandishi alikuwa anaumia sana rohoni siku mbili hizi hajatoa taarifa ya kipenzi chake

    ReplyDelete
  3. Hata mkifanya nini, kwa Simba hii ya Moo, ubingwa mtaungojea sana

    ReplyDelete
  4. Mwandishi andika pia kuhusu kipigo alichopokea Yanga kutoka KMC na Kagera. Vipi muuaji wa Yanga kutoka KMC?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic