April 11, 2020

 UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa umewatumia fedha wachezaji wao wawili, Yakub Mohamed na Razack Abarola kutokana na kushindwa kurejea nchini kwa sasa.

Wachezaji hao walikuwa kwao Ghana kwa ajili ya mapumziko kufuatia Ligi Kuu Bara kusimama kwa muda.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Azam FC, Zakaria Thabith amesema kuwa kutokana na ugumu huo hawajui ni lini nyota hao wanaweza kurudi nchini.

“Unajua hali ya maambukizi katika nchi ya Ghana imekuwa kubwa kiasi cha Serikali kutangaza hali ya tahadhari kwa kuwataka wananchi wote kubaki nyumbani kwao.

“Tumewasiliana nao na wametuambia hata vituo vya kufanyia mazoezi vimefungwa, hivyo imebidi tuwatumie fedha kwa ajili ya kununua vifaa vya mazoezi ambavyo vitawasaidia kuendelea na mazoezi wakiwa ndani.

“Hatuwezi kufanya lolote kwani hata safari za ndege zimefutwa, tunasubiria kuona ni jinsi gani hali ya mambo inaweza kuwa baada ya janga hili kupita,” amesema Thabith.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic