UONGOZI wa Simba umesema kuwa mpango mkubwa kwenye kuboresha kikosi chao kwa sasa ni sehemu ya mshambuliaji ili kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho.
Wakati Ligi Kuu Bara inasimamishwa kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona, safu ya ushambuliaji ya Simba ilikuwa inaongoza kwa kutupia mabao ambao ilikuwa imefunga mabao 63.
Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema kuwa kuna ulazima wa kuongeza washambuliaji ili kuwa na mbadala pale ambapo mmoja akipata matatizo.
"Nilianza kukinoa kikosi nikiwa na mshambuliaji tegemezi mmoja ambaye yeye alikuwa fiti huku wengine wakiwa ni majeruhi, kwa sasa malengo yangu ni kuona kwamba kila nafasi inakuwa na mbadala wake jambo linalofanya nihitaji kuwa na washambuliaji zaidi.
"Hiyo itasaidia iwapo itatokea kutakuwa na wagonjwa ama tatizo lolote lile wao wataendelea kucheza bila hofu ila hawa waliopo pia wanafanya kazi kubwa," amesema.
Miongoni mwa washambuliaji ambao wanatajwa kuwindwa na Simba ndani ya Bongo ni Relliants Lusajo anayekipiga ndani ya Namungo akiwa na mabao 11 pamoja na Paul Nonga anayekipiga Lipuli.







Ndio mbili tu wala si kikosi kamili cha huyu anapotia nazi mwengine inaimimina chumvi
ReplyDeleteSasa naona kweli Simba hawana nia ya kutoka hapa walipo au walipoishia championship league na kufika mbali zaidi kama vile wamekata tamaa.Kikosi cha Simba hasa sehemu ya beki na washambuliaji wa kati hakijafanyiwa marekebisho yeyote. Akina lusajo sijui Nonga kwa Simba sawa lakini wasisahau walikuwa nae Adam salamba,Kaheza,Mo Rashid waliwika vijijini ila walipotua mjini wakawa nyanya. Waswahili walishasema maneno kuntu kabisa yakwamba karamu ya mbahili huliwa mara mbili yaani hasara baada ya kusevu.Nnaamini kama pesa za usajili za Adam salamba,Mo Rashid,Kaheza,mbrazili na huduma nyengine za kuwahudumia zingetumika kutafuta mchezaji mmoja wa maana kaliba ya akina Bwalya leo hii Simba wangekuwa wanacheka au wanasubiri ofa kubwa kutoka timu fulani kumuuza kwa mchezaji huyo kwa bei kubwa zaidi. Mfano kotei sawa kurudi Simba ila Simba wanahitaji kiungo bora zaidi ya kotei ili kukua kutoka walipo sasa kiungo amabe hata wakitaka kumuuza timu kubwa anauzika bila kigugumizi.
ReplyDeleteHizo ni stori tu za kujifurahisha. Mipango ya Simba kwenye usajili inafanyika chinichini kwa siri. Hayo majina sijui mnayatoa wapi!
DeleteKama kawaida usajili wa magazetini ndio umeshaanza. Ni wakati sasa wa magazeti kupiga pesa ndefu hasa ukizingatia ligi zimesimamaishwa karibia duniani kote waandishi na watangazaji wa habari za michezo hawana jipya la kuripoti.
ReplyDelete