LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa nafasi yao ya kutwaa ubingwa ni ndogo kutokana ushindani uliopo ndani ya Ligi Kuu Bara huku akiachwa pointi nyingi na mpinzani wake Simba.
Kwa Sasa Ligi Kuu Tanzania Bara imesimamishwa kwa muda kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona ambapo Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 71 huku Yanga ikiwa na pointi 51 nafasi ya tatu.
Eymael amesema kuwa bado kuna ugumu wa timu yake kuchukua ubingwa kutokana na kuachwa kwa pointi nyingi na mpinzani wake.
“Kwa sasa bado ni ngumu kusema kwamba tuna nafasi kubwa ya kuwa mabingwa labda kwa wakati ujao, ninaona wapinzani wetu wametuacha kwa idadi kubwa ya pointi jambo ambalo ni kizuizi cha kwanza.







Ikiwa nyumba za ibada zinatumika kwa ibada kikamilifu na wananchi kama kawaida Kutoka kujitafutia maisha, ligi pia inaweza kuendelea hata pindi Bila ya mashabiki almuradi apatikane bingwa na zijulukane timu zilizoshuka na za kuupanda daraja Bila ya masononeko
ReplyDeleteNahisi shida ni kusafiri timu na benchi la ufundi
ReplyDelete