May 8, 2020


THABIT Zakaria, Ofisa Habari wa Azam FC amesema kuwa hakuna tatizo iwapo Ligi Kuu Bara itarejea na kuchezwa bila mashabiki kwa kuwa imetokea ikiwa ni dharula.

Ligi ilisimamishwa Machi 17 kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona na Serikali kupitia kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuna uwezekano ikarejea Juni ila Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema kuwa itachezwa bila mashabiki na watategemea kauli ya Serikali.


 "Kucheza ligi bila mashabiki hiyo ni kama dharula imetokea hakuna namna ya kupinga kwa sasa ni sawa ukiwa vitani huchagui silaha kikubwa ni kupambana. 

"Mashabiki watulie nyumbani watapata taarifa kupitia vyombo vya habari," amesema.

Azam FC ipo nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 54 kibindoni baada ya kucheza mechi 28.

1 COMMENTS:

  1. Tunaomba Azam kutokana na umaarufu wa ukarimu wa viongozi wake, ituwezeshe nasi wapenzi wa soka kuziona mechi hizo kwa njia itayoonekana muwafaka

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic