May 18, 2020


UONGOZI wa Klabu ya Azam FC umesema kuwa baada ya ukarabati wa sehemu ya kuchezea (pitch) kukamilika vizuri, sasa Azam FC imeanza rasmi kukarabati majukwaa ya mashabiki kwenye uwanja wa Azam Complex.

Azam FC imesema tayari mafundi wameanza kutoa mbao zilizochakaa kwenye majukwaa yote ndani ya Azam Complex, kabla ya kumalizia na zoezi la kuweka mbao mpya katika sehemu za kukalia za mashabiki.


Azam FC ilianza ukarabari wa uwanja wake mwishoni mwa mwaka jana ambapo wakati wa maboresho hayo walikuwa wakitumia uwanja wa Taifa na Uhuru.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic