MAALIM Busungu, mshambuliaji wa zamani wa Yanga amesema kuwa kwa sasa ni muhimu kila mmoja akachukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.
Busungu amesema kuwa hali inaweza kuwa salama iwapo kila mmoja akachukua tahadhari dhidi Corona na kujilinda yeye kwanza na jamii kiujumla.
"Kwa kipindi hiki kigumu ambacho tunapitia ni muhimu kila mmoja akachukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona kwani ni janga hatari ambalo linaitikisa dunia.
"Iwapo kila mmoja akachukua tahadhari itakuwa rahisi kwake kujilinda na kuwalinda wengine, yale maelekezo yanayotolewa na Wizara ya afya pamoja na Serikali yasipuuzwe," amesema.
Habari iko nusu, haijaeleza kwa sasa Busungu yuko wapi na anafanya nini, maana kweli ni mshambuliaji wa Yanga wa zamani, lakini Leo hii yuko wapi, msaada please
ReplyDelete