INAELEZWA kuwa uongozi wa Simba ulikuwa kwenye vita nzito ya kuwania saini ya mshambuliaji wa Asante Kotoko ya Ghana, Yacouba Songné, raia wa Burkina Faso lakini mshambuliaji huyo amepiga chini ofa hiyo na kujiunga na Medeama ya nchi hiyo kwa dau la Sh milioni 344.
Medeama imefanikiwa kumsajili nyota huyo mwenye uwezo mkubwa wa kufunga huku akizipiga chini Orlando Pirates ya Afrika Kusini, Al Hilal ya Sudan, Inter Allies ya Ghana na Simba ya Tanzania.
Simba ilikuwa ikimhitaji mshambuliaji huyo kutokana na mapendekezo ya kocha mkuu wa timu hiyo, Mbelgiji, Sven Vandenbroeck aliyependekeza usajili wa washambuliaji wapya katika kikosi chake kwa lengo la kusaidiana na Mnyarwanda, Meddie Kagere na nahodha John Bocco.
Mwenyekiti wa Asante Kotoko, Dk Kwame Kyei, amekiri kuondoka kwa mshambuliaji huyo kwa dau la dola 150,000 sawa na Sh milioni 344 kutokana na kushindwa kufikia dau hilo.
“Songne ameonda kwenye klabu yetu kama mchezaji huru katika usajili uliokamilika mwezi uliopita, alikuwa ni mchezaji mzuri ambaye bado klabu ilikuwa ikimhitaji lakini tusingeweza kuwa naye kutokana na kutaka tumpe dola 150,000, pesa ambayo klabu haikuwa nayo.
“Kiukweli kwetu ni masikitiko lakini tusingeweza kuwadanganya mashabiki kama ataendelea kuwepo kwetu wakati tumeshindwa kufikia mahitaji yake ambayo alikuwa akiomba yatimiziwe katika mkataba mpya, hasa upande wa dau,” alisema Dk Kyei.








hiyo habari no ya uongo mkubwa sababu Medeama na Songne walishindwa kufika makubaliano na tarehe 12 mweneyekiti was Medeama alitangaza rasmi kujitoa kumuania Songne na kuchukua mchezaji mwingine kwa gharama ndogo. Na hate huyo Mbukina yupo yupo tu hapa Accra Ghana Tena hana timu na alikuwa majeruhi hakucheza mechi zote 5 za mwisho za Asante Kotoka anaangaika kutafuta timu bar Asia. Kijarida chenu kiache kuandika uongo na kuwadanganya wapenda habari za michezo. Habari za kweli kuhusu Mambo ya Ghana munaweza kuzipata kwenye mitandao ya michezo ya Ghana sio kijarida hicho Cha Sakehe Jembe Cha habari uongoza kutunga na Kila siku kinaandika habari zile zile na nyingi za uongo
ReplyDeleteHadhi ya hiki kijarida inapungua siku hadi siku.Uzushi,mapenzi nä kukosa weledi vimewaponza. Wamekuwa wazushi bila uandishi wa uhakika.
ReplyDelete