May 30, 2020


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa umejipanga kwa ajili ya kuanza safari ya mabadiliko una amini kila kitu kitakamilika kwa wakati kwa kuwa hawajakurupuka na kuwaomba mashabiki wasikose kufuatilia kesho kuona mambo mazuri ambayo yameandaliwa na La Liga pamoja na kampuni ya GSM.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Uhamasishaji na Msemaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa kila kitu kipo kwenye mipango mizuri jambo linalowapa imani ya kufikia malengo ambayo wameyapanga.

“Tupo vizuri na tunapambana kuelekea kwenye safari ya mabadiliko, Mei 31 itakuwa ni hatua ya kutiliana saini kati ya Yanga, GSM na La Liga kutoka Hispania hivyo ni fursa kwa mashabiki kufuatilia kwa umakini na kuona mambo ambayo yatajadiliwa.

 “Mashabiki watatu watawakilisha wengine wote ambao watatazama moja kwa moja matangazo kupitia Azam TV  na Yanga TV  kuanzia saa moja usiku, kuna makubwa ambayo watayaskia na yatawafurahisha, hivyo wasikose kuna mambo mazuri yanakuja,” amesema Nugaz.

Yanga imeanza safari ya kuelekea kwenye mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji ikiwa ni ndoto ya wengi wakiongozwa na Mwenyekiti wa Klabu hiyo Mshindo Msolla.

1 COMMENTS:

  1. Mpira pesa tunawatakia Kila la kheri ktk sfr ya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaj wa klabu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic