KEVIN De Bruyne, kiungo mtengeneza mipango ndani ya Klabu ya Manchester City amesema anaweza kusepa ndani ya klabu hiyo iwapo haitafunguliwa adhabu yao ya kufungiwa miaka miwili kutoshiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Shirikisho la Soka Ulaya,(Uefa) liliifungia City, kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya mwezi Februari mwaka huu kutokana na kukiuka kanuni za mapato na matumizi.
Kiungo huyo mwenye miaka 28 yupo kwenye ubora wake ambapo ametoa jumla ya pasi 16 za mabao msimu huu ndani ya City amesema kuwa hatma yake ndani ya klabu hiyo inategemea matokeo ya rufaa iliyokatwa na mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu England.
Kiungo huyo amesema kuwa kukaa miaka miwili bila kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya ni mingi labda ingekuwa mwaka mmoja.
"Miaka miwili bila kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya ni mingi labda ingekuwa ni mwaka mmoja angalau kidogo tutasubiri na kuona kitakachotokea," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment