May 6, 2020


WINGA machachari wa Yanga raia wa Ghana, Bernard Morrison ameanika wazi uwezo wake wa kumshawishi Justin Shonga wa Orlando Pirates kuungana na kikosi cha Yanga, endapo viongozi wa timu hiyo watakuwa tayari kumpatia kiasi cha fedha alichokiomba.

Morrison ni moja ya wachezaji wa Yanga ambao wamejiunga na kikosi hicho wakati wa dirisha dogo la usajili lililopita, kwani kabla ya kuja Yanga, aliwahi kuichezea Orlando Pirates, lakini tayari ameshakuwa na ushawishi mkubwa ndani ya timu yake ya sasa hasa baada ya kuisaidia kushinda dhidi ya Simba na kumfanya afikishe mabao matatu kwenye Ligi Kuu Bara.

Morrison ameendelea kusisitiza kwa kusema kuwa, yuko tayari kuisaidia Yanga kwenye maongezi yao na Shonga, maana ni mchezaji ambaye wanafahamiana vizuri tangu alipokuwa Orlando Pirates, ila kikubwa kama Yanga watakuwa tayari kutoa dau analolitaka tu.

“Kweli nimekuwa nikisikia tetesi nyingi sana hapa Tanzania, hasa Simba wakihusishwa kumtaka Shonga na kwamba kuna muda niliona sehemu kama Shonga na timu yake wapo tayari kumuachia kwa dau la milioni 800, jambo ambalo mimi nadhani ni mchezaji anastahili kwenye ligi hii.

“Nipo tayari kwa timu yoyote kuwasaidia kuzungumza naye, maana ni muda mrefu sasa naona kama hana nafasi sana kwenye kikosi cha kwanza japo uwezo wake ni wa hali ya juu sana.

“Nadhani kama Yanga wao wakimuhitaji na kuniambia wapo tayari kumpatia dau atakalohitaji mimi sina kipingamizi cha kuwasaidia kwani akija hata kwangu ni msaada mkubwa,” alisema Morrison.

Chanzo: Championi

1 COMMENTS:

  1. Sasa nyie Yanga si mnao wachezaji wa kigeni zaidi ya ishirini mliowataja wenyewe huyo Shonga wanini tena?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic