May 6, 2020


HENRICK Chota, mwanachama wa Yanga ambaye aligombea nafasi ya Umakamu Mwenyekiti kwenye uchaguzi wa Yanga mwaka jana, 2019 amesema kuwa miongoni mwa wachezaji anaowakubali kutoka ndani ya Klabu ya Simba ni pamoja na Clatous Chama, Deo Kanda na Meddie Kagere.

Chota amesema kuwa kabla ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona alikuwa anawafuatilia kwa ukaribu wapinzani wao ambao anaamini kuwa wana kikosi kipana na kizuri kama ilivyo kwa Yanga.

"Ninapenda uwezo wa nyota wengi wa Simba ila hawa watatu ambao ni Clatous Chama, Deo Kanda na Meddie Kagere ninawakubali.

"Simba ina kikosi kizuri kama ilivyo kwetu ila tumewazidi kwenye upande wa burudani kwani ilionekana Machi 8, kuna rafiki yangu alikuwa wa Simba alinipa tabu sana siku hiyo uwanjani," amesema.

Yanga iliwatungua Simba bao 1-0 kwenye mchezo wa mzunguko wa pili uliochezwa Uwanja wa Taifa.

3 COMMENTS:

  1. burudani ipi ya kuchezesha majini uwanjani

    ReplyDelete
  2. Hawa Utopolo toka wabahatishe kuifunga Simba kwao ni kama kuchukua Ubingwa wa Afrika wanamuona huyo Morison kama Mungu wao wametumia milioni 200 kwa ajili tu ya kuifunga Simba inaonesha jinsi gani Simba ilivyokuwa fupa gumu kwao kila kukicha lazima ushindni wao huo wa kubahatisha wauzungumzie kwa namna moja au nyingine kweli Simba chama kubwa lakini wasisahau huu mpira bado mechi zipo nyingi zakutosha muda si mrefu tutawasababishia mgogoro tuombe Mungu CORONA iishe.

    ReplyDelete
  3. Kila wanaposikia Mnyama Ana mazungumzo na mchezaji fulani Mara huruka na wao kumtaka kweli wana ubavu hawa jamaa wa kumpiga pushi na kuuweka upande MOOO ili usukani waukamate waooo. Wa kale walisema "mwenye nguvu mpishe kama hujampisha atakupiga kigumbo"

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic