May 26, 2020


UKISIKIA ngoma hii ambayo haikosekani kwenye laptop za MA-DJ, lazima utauliza inaitwaje na ni ya mwanamuziki gani?

Usipate taabu. Ngoma inaitwa Unanikosha. Ni ya dogo mmoja ambaye kwa sasa ni moto wa kuotea mbali, wanamuita Toto Bad. Wengi tunamjua kama Marioo.

Jina kamili ni Omari Ali Mwanga. Ni bonge moja la kipaji kilichojaa utunzi wa mashairi na melodi tamu ndani yake.
Mbali na Unanikosha, Marioo anasikika vizuri mno kwenye midundo ya ngoma zake kali kama Raha, Aya, Manyaku, Ifunanya, Inatosha, Anyinya na nyingine kibao ambazo zimetazamwa na mamilioni kwenye YouTube.

Nikukumbushe tu, Marioo kabla ya kuingia kwenye tasnia hii, alipata vikwazo vingi katika safari yake ya muziki, wakati huo akiwa fundi magari kwenye gereji.

Inatosha, ni ngoma yake ambayo bado inasikika na kuteka vichwa vya mashabiki wa muziki wa Bongo Fleva.

Marioo amesema kuwa anashukuru kwa sapoti ya mashabiki ambao wamekuwa naye bega kwa bega anaamini mengi yanakuja na ataiongeza juhuhudi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic