KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vanderbroeck amesema kuwa ni ngumu kwa sasa kwa nyota wake Sharaf Shiboub kujiunga ndani ya kikosi chake kutokana na ugumu wa sheria zilizopo nchini kwao.
Shiboub kwa sasa yupo nchini Sudan, ambapo aliibuka huko baada ya Serikali kusimamisha masuala ya michezo Machi 17 kutokana na janga la Corona ambalo linaivurugavuruga dunia.
Kwa sasa, tayari Serikali imeruhusu masuala ya michezo kuanza ifikapo Juni Mosi baada ya hali ya maambukizi ya Corona kupungua.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Sven amesema kuwa kuna ugumu wa kumpata Shiboub kutokana na mazingira yalivyo.
"Shiboub yupo kwenye nchi ambayo imekuwa na sheria ngumu na mipaka imefungwa kutokana na janga la Corona hivyo ni ngumu kwake kuweza kurejea kwa wakati.
"Bado tunaendelea kuwasiliana naye ili kujua ni namna gani anaweza kuja nchini kujiunga na wenzake," amesema.
Shiboub ndani ya Ligi Kuu Bara amefunga mabao mawili na kutoa pasi sita kati ya mabao 63.
0 COMMENTS:
Post a Comment