May 26, 2020


SELEMAN Mataso, Mwenyekiti wa Klabu ya Biashara United ameshukuru kupokea msaada wa mipira 19 kutoka kwa Uongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Musoma mkoani Mara.

Msaada huo ni kwa ajili ya kuipa sapoti timu hiyo kwenye maandalizi ya kukamilisha mechi tisa zilizobaki.

 Mataso amesema, "Tulikuwa na hali mbaya sana katika suala la mipira hivyo huu msaada utatusaidia kwa kiasi kikubwa sana katika mazoezi yetu,".

Kwa upande wa Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Musoma Benedict Magiri amesema michezo ni sehemu ya sera ya chama hicho hivyo msaada huo ni sehemu ya kutekeleza Ilani ya chama hicho.

Tayari kikosi cha Biashara United Mara leo kimeanza mazoezi rasmi kipo nafasi ya 10 baada ya kucheza mechi 29 ikiwa na pointi 40.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic