PACHA ya
mabeki wawili wazawa ndani ya Simba, Mohamed Hussein na Shomari Kapombe imejibu
baada ya nyota hao kuhusika kwenye mabao tisa ya timu yao licha ya kuwa ni mabeki.
Kapombe
ambaye ni beki wa kulia amehusika kwenye mabao matano huku Tshabalala akihusika
kwenye mabao manne kati ya 63 yaliyofungwa.
Tshablala
amefunga mabao mawili na kutoa pasi mbili za mabao ambapo pasi yake ya mwisho
kabla ya ligi kusimamishwa alimpa Meddie Kagere mbele ya Singida United wakat
Simba ikishinda mabao 8-0.
Kapombe naye
akiwa ametoa pasi tano, pasi yake ya mwisho alimpa Kagere Uwanja wa Taifa
wakati Simba ikishinda mabao 3-2.







0 COMMENTS:
Post a Comment