BAADA ya PSG
kutangazwa kuwa ni mabingwa wa Ligi Kuu Ufaransa ‘Ligue 1’, beki na nahodha wa
timu hiyo, Thiago Silva, ameugawa ubingwa huo kwa madaktari dunia nzima.
Hivi karibuni,
PSG walitangazwa kuwa mabingwa wa Ligue 1, baada ya kufahamika kuwa ligi hiyo
haiwezi kuendelea tena kwa msimu huu.
Kutokana na
madhara ya virusi vya Corona ambavyo vimevamia dunia nzima kwa sasa, Ufaransa
wao wametangaza kuwa ligi hiyo imefutwa kwa kuwa serikali ya nchi hiyo imesema
kuwa michezo itaruhusiwa kuendelea tena, Septemba mwaka huu.
Silva
amesema ubingwa huo ni kwa ajili ya madaktari wote ambao wanapambana na virusi
vya Corona duniani kote kwa kuwa wanafanya kazi ngumu sana na hatari.
Wakati ligi
hiyo inasimama Machi, mwaka huu kabla ya msimu kuahirishwa kabisa, PSG walikuwa
mbele kileleni kwa tofauti ya pointi 12 na mchezo mmoja mkononi.
“Huu ubingwa
unabaki kuwa alama tosha kwenye mafanikio yetu.
“Ninachoweza
ni kumshukuru Mungu kwa kutwaa ubingwa wa saba katika miaka nane niliyokaa Ligue
1.
“Hakika
nisingeweza kufika hapa kama siyo sapoti ya familia, lakini hakika ubingwa huu
ni maalum kwa ajili ya madaktari wote duniani ambao wanapambana na virusi vya
Corona,” aliandika beki huyo raia wa Brazil katika akaunti yake ya Instagram.
0 COMMENTS:
Post a Comment