May 30, 2020


MASAU Bwire, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mechi zao zote 10 zilizobaki kuendelea kutoa burudani kwa mashabiki wao.

Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea kutimua vumbi Juni 13 ambapo ilisimama tangu Machi 17 kutokana na janga la Virusi vya Corona.

Akizungumza na Saleh Jembe, Bwire amesema kuwa walikosa kuendelea kutoa burudani kwa muda mrefu na kwa sasa wanaamini watwapa mashabiki kile walichokikikosa.

"Kuna mambo ambayo yalitokea hapo nyuma najua kila mmoja anajua ilikuwa ni janga la Corona, kwa kuwa kwa sasa hali imeanza kuwa shwari kwa mujibu wa Serikali tunaamini ni wakati wetu wa kuendelea pale tulipoishia.

"Wachezaji wapo tayari kuendelea kupambana na tuna imani kwamba kazi kubwa itakuwa kwenye kutafuta matokeo hilo lipo kwa wachezaji baada ya kupata maandalizi mazuri," amesema.

Ruvu Shooting ipo nafasi ya 11 ikiwa imecheza mechi 28 kibindoni ina pointi 39.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic