May 4, 2020


ERASTO Nyoni, beki kiraka ndani ya Simba amewaomba watanzania kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.
Nyoni amesema kuwa kwa sasa ni muhimu kila mtanzania kuwa balozi kwa mwenzake kwani janga hili linamhusu kila mmoja.
“Ninaamini kwamba kila mmoja anatambua kwamba kwa sasa mambo mengi yamesimama kutokana na uwepo wa janga hili la Corona hivyo ni vizuri ikiwa kila mmoja atachukua tahadhari.
“Mimi nimeanza ambapo nikiwa nyumbani ninawakumbusha wale wanaonizunguka kunawa na kuvaa barakoa ninapenda kuona na watanzania wengine wakazidi kuwa mabalozi ili tuishinde vita hii,” amesema Nyoni. 
Kwenye mabao 63 yaliyofungwa na Simba, Nyoni amefunga bao moja kwa kichwa ilikuwa mbele ya Azam FC Uwanja wa Taifa.

1 COMMENTS:

  1. Tunaambiwa miongoni mwa nchi ambazo zimeishinda corona kwa kipigo cha aibu basi ni Taiwani. Licha ya kuwa miongoni mwa sehemu ya China kwa ukaribu wa masafa na uhusiano wa kidugu,tunaambiwa Taiwani licha ya shuguli za maisha kundelea kama kawaida lakini ni miongoni nchi zilizofanikiwa sana kuidhibiti corona na kugeuza corona kama fursa ya kichumi kwa kutengeneza na kuuza vifaa vingi vya kupambana na corona hadi kuisadia mpaka Marekani. Wataiwani kwa kufuata miiko na maelekezo ya viongozi wao wakuu wa nchi wameweza kufanya maajabu katika kupambana na corona na hapa ndipo ninapotaka kuchukua fursa hii kuwashika sikio watanzania kwa umakini mkubwa kabisa yakwamba kama bado tumelala usingizi basi tunapaswa kuamka kutoka kwenye usingizi huo kwa kishindo. Na kitu gani hicho kitakachowafanya watanzania kumka kwa kishindo? Hakuna kingine bali ni Kiongozi wetu mkuu wa nchi muheshimiwa John Magufuli. Huyu jamaa ni zaidi ya ya rasilimali watu,huyu jamaa ni dhahabu na watanzania tuna hiyari yetu ya kwa kiasi gani tutaitumia dhahabu hii kujikomboa na umasikni na unyonge katika taifa letu .Kuna vioja vingi vinaendelea kufanywa nje na ndani ya nchi yetu kumtoa Magufuli mchezoni.Lakini kama kuna timu duniani inaweza kushinda kwa umahiri wa team kapteni wake basi ni timu Tanzania na hapa nazungumzia hasa katika masuala ya maendeleo ya nchi yetu. Watanzania wakijua thamani ya Magufuli watashinda sio corona tu bali wanaweza kufanya maajabu kwenye mambo mengi na kuishangaza Dunia. Kiuhalisia Magufuli yupo vitani tangu day one alipoingia madarakani na hata hii corona ilipofika ilimkuta Magufuli yupo vitani kitambo na ndio maana kwake yeye binafsi Magufuli corona haikuwa taharuki ila kwa watanzania wengi imetukuta corona bado tumelala fofo na ndipo hapa unapogundua madhaifu makubwa kabisa ya watanzania ya kutoendana sambamba na kasi na utayari wa aina ya Kiongozi wao mkuu katika kulipigania taifa. Binafsi nampongeza sana muheshimiwa John Magufuli kwa msimamo wake imara na thabiti kwenye janga hili la Corona.Naishi ya nje ya nchi ila kama walivyo watanzania wa diaspora kiakili huwa tupo nyumbani kila mara na ningependa salamu hizi zimfikie muheshimiwa John Magufuli . Vita watu watakufa ila hakuna vita inayoshindwa kwa kujifungia ndani na huko ni kumkabidhi adui mamlaka ya kukushinda na kukumaliza.vita yeyote Duniani inapiganwa na vijana na kama vijana hao watakuwa wazembe na waoga basi wata hatarisha maisha ya wazee,watoto na wagonjwa.Ninachotaka kusisitiza hapa hasa kwa vijana wa kitanzania tusii hukulie poa hii vita ya corona hata kidogo kila mmoja atimize wajibu wake ipasavyo na kwa uwezo wa Mungu vita hii tutashinda. Na kwenye vita maafa ni lazima la sivyo isingeitwa vita la msingi hapa ni kufuata maelekezo ya jemedari wa vita na kwa bahati nzuri jemedari wetu wa vita yupo vizuri sana,He is not a coward man hes a war hero tumuunge mkono. .

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic