May 3, 2020


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa njia bora ya kumpata bingwa wa Ligi Kuu Bara ni mpira kuchezwa uwanjani ikishindikana basi matokeo yote yafutwe ili kuanza upya.

Kwa sasa ligi imesimama kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona ambavyo ni janga la dunia nzima ambapo wakati inasimishwa Yanga ilikuwa nafasi ya tatu na pointi zake 51.

Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa:-"Njia bora ya kumpata bingwa ni uwanjani ambapo mechi zikichezwa inakuwa rahisi kumpata bingwa kwani kwa sasa kinara akipewa kombe atakuwa anatuonea sisi pia tuna nafasi ya kuwa mabingwa.

"Tuna mechi za viporo hatujacheza na kikosi kilikuwa kinachanganya, majirani zetu Kenya hata ukiangalia Angola walikuwa wana kanuni za dharula lakini sisi hilo halipo hivyo itapendeza bingwa atafutwe uwanjani ama msimu ufutwe kusiwe na bingwa," amesema.

Kinara wa ligi ni Simba ana pointi 71 kibindoni baada ya kucheza mechi 28.

7 COMMENTS:

  1. Kipolo kimoja ndio kikufanye uwe bingwa? Itakuwa ni kutaka tukose wote badala ya kuangalia hali halisi. Basi wapewe yanga

    ReplyDelete
  2. Ha ha ha ha wapewe yanga chap kwa haraka maana kombe likienda simba kutakua na hasara kubwa sana.kwa yanga na serikali yao.angalia wanavyotoa povu.na kama haiwezekani kupewa basi waachiwe nafasi yakucheza klabu bingwa afrika.GOR MAHIA wamepewa kombe lao na nchi kibao za Afrika klabu zilizokua zinaongoza ligi zimepewa kombe lao,sasa kwanini Tanzania tusiige huko tumejawa na ushabiki baada yakuangalia uhalisia wa jambo?ninachokiona mimi hapo timu zote zingebalance mechi kwa maana either wenye viporo wapewe nafasi wacheze ili walingane na wengine au wale waliozidi mechi wafutiwe mechi za mwisho walizocheza ili timu zilingane maana yanga wanatafuta sababu wapate kuongea.

    ReplyDelete
  3. Hapa ndipo ambapo hua naona vioja sijajua ni waandishi au ni viongozi
    Gazeti la mwanaspoti liliwahi mnukuu kiongozi ws Yanga akitaka ligi ifutwe leo tena kiongozi mwingine wa Yanga anapinga hilo kwani ligi ikifutwa na ikaamriwa matokeo yalivyo yabaki hivyo hivyo wanakosa nini

    ReplyDelete
  4. Hawa jamaa matata Sana eti ligi ivunjwe kabisa na Kuanza upya. Hasadi mbaya Sana no kama moto kama haijapata cha kukiunguza hujiunguza mwenyewe

    ReplyDelete
  5. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  6. Ikiwa mnangoja ligi na matokeo yake yafutwe na ianze upya basi mmechelewa kabisa na hata pindi ikiwa ni hivo basi muusahau hasa ilivokuwa timu yenu yote mpya hasa ilivokuwa mnasajili zaidi ya nyota ishirini wakigeni

    ReplyDelete
  7. Kweli kiongozi kama huyo anatoa kauli hivyo, unategemea ataongoza au atapotosha?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic