UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa hesabu zake kwa sasa ni kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa Juni 21, Uwanja wa Taifa dhidi ya Yanga.
Azam FC iliyo chini ya Kocha Mkuu, Aristica Cioaba ilianza pale ilipoishia kwenye ligi kwa kushinda mabao 2-0 mbele ya Mbao FC mchezo uliochezwa Juni 14, Uwanja wa Azam Complex.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit, amesema kuwa ushindi wao mbele ya Mbao wanauacha na kutazama mechi zinazofuata ikiwa ni pamoja na Yanga.
“Bado mapambano yanaendelea na tutazidi kujiweka sawa ili kupata ushindi kwenye mechi zetu zilizobaki ili kuona tunafikia malengo. Ushindi wetu mbele ya Mbao FC ni chachu kwetu kujiandaa kwa ajili ya Yanga, tupo tayari,” amesema Thabit.
Azam FC ipo nafasi ya pili baada ya kucheza mechi 29 kibindoni ina pointi zake 57.
0 COMMENTS:
Post a Comment