June 20, 2020


HASSAN Bumbuli, Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga amesema kuwa wana mahusiano ya ukaribu kikazi na Ofisa Habari wa Simba Haji Manara.
Bumbuli anasimamia kitengo cha Habari ndani ya Klabu ya Yanga ambapo mpinzani wake mkubwa ni Haji Manara anayesimamia kitengo cha Habari cha Simba. 
Mabosi hawa wamekuwa wakitumiana maneno kwa kila mmoja kulinda nembo ya timu yake kwa wakati wake.
Bumbuli amesema kuwa:“Uhusiano wetu na Haji Manara upo,sawa kwenye masuala ya kikazi licha ya kuwa huwa kunaotkea tofauti za hapa na pale.
“Ipo wazi katika hilo hasa tunapokuwa kwenye kazi, ila naona yeye anataka kuwashambulia wenzio ila yeye hataki, hiyo sio sawa lazima akubaliane na hali halisi kwani ukiwa unashambulia nawe ni lazima ukubali kushambuliwa.”

5 COMMENTS:

  1. Kumshambulia ndo amtukane au ambague kutokana na rangi yake mwambie aache ujinga yaani huyo bumbuli hana tofauti na polisi wa marekani

    ReplyDelete
  2. Bumbuli mshamba.Hajui asili ya utani wa Simba na Yanga. Amekuja kutoka kijijini anafikiri utani wa Simba na Yanga ni matusi.Simba nä Yanga wanataniana hadi kwenye misiba na ndoa ,shida nä raha Ukiwa mjuka huwezi kuelewa utani huo.Inabidi viongozi wakuja wa klabu hizi wapewe semina ya asili ys utani huo.Matusi na unyanyasaji hauna nafasi kwenye utani huu.

    ReplyDelete
  3. Utani ulenge klabu na si mtu binafsi, aitumie Simba kama Simba lakini utu wa mtu. Manara yeye alicheza gari ya Yanga na si mtu, Bumbuli anaongeleaje Albinism ni unyanyapaa unaotakiwa kukemewa

    ReplyDelete
  4. utani ulenge simba na yanga si matusi

    ReplyDelete
  5. Mtaipata freshi na huyo mwehu wenu kumi hazichangui pakupiga kwahiyo ukijona mdhaifu acha ungomvi usitumie mapungufu yako ya kimaumbile kama kinga yako utapewa vitu hongera sana mbumbuli

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic