JKT Tanzania, leo imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Yanga kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
Mchezo wa leo ulikuwa na ushindani mkubwa ambapo JKT Tanzania ilianza kupachika bao la kuongoza dakika ya 36 kupitia kwa Michael Aidan aliyemtungua Metacha Mnata kwa guu lake la kulia akiwa nje ya 18.
Iliwalazimu Yanga kusubiri mpaka dakika ya 76 kusawazisha bao hilo kupitia kwa Patrick Sibomana aliyefunga bao hilo baada ya kipa wa JKT Tanzania kutema mpira uliopigwa na Haruna Niyonzima.
Mpaka dakika 90 zinakamilika wachezaji wawili walionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 88 ambapo kwa Yanga, Lamine Moro alionyeshwa kadi hiyo huku wa JKT Tanzania, Mwinyi Kazimoto akionyeshwa kadi hiyo dakika ya 88 baada ya mwamuzi kutafsri kuwa walifanya vitendo visivyo vya kuungwana uwanjani.
Matokeo hayo yanaifanya Yanga ifikishe jumla ya pointi 55 ikiwa nafasi ya tatu huku JKT Tanzania ikifikisha pointi 43 ikiwa nafasi ya 7.
Daaah!!!! maneno yameishia wapi sijui? Poleni Jangwani michezo sawa sasa hakuna kisingizio.
ReplyDelete