NAHODHA msaidizi wa kikosi cha Yanga, Juma Abdul Mnyamani amefunguka kuhusu michoro ya mwilini ‘Tatoo’ aliyo nayo kwa kusema kuwa michoro hiyo imemgharimu kiasi cha shilingi laki nane za kitanzania kuikamilisha huku pia akieleza maana mbalimbali za michoro hiyo.
Akizungumza na Saleh Jembe,Juma Abdul amesema michoro hiyo ni maalumu kwa ajili ya watu wake wa karibu hasa wazazi wake na mtoto wake.
“Nimechora michoro tofauti sita mwilini mwangu ambayo kwa ujumla wake imenigharimu kiasi cha shilingi laki nane za kitanzania ili kuikamilisha, kifuani nimechora michoro miwili ya maandishi kwa ajili ya wazazi wangu ambayo ilinigharimu laki mbili na nusu.
“Mkono wa kulia nina michoro mitatu, miwili ikiwa ni picha ya mama yangu na mwanangu na moja ya maandishi zote ziligharimu shilingi laki nne na nusu na mkono wa kushoto kuna mchoro mmoja wa ua ulionigharimu shilingi laki moja,” amesema Abdul.
Nahodha huyo msaidizi wa Yanga amehusika kutoa pasi tano za mabao kati ya 31 yaliyofungwa na Yanga msimu huu.
0 COMMENTS:
Post a Comment