JONAS Mkude,
kiungo mshambuliaji wa Simba amewekwa kwenye uangalizi maalumu wa jopo la
madaktari kwa ajili ya kumfanyia uchunguzi wa jeraha lake la mguu alilopata
jana, Juni 8 kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya KMC.
Mkude
aliumia kipindi cha pili kwenye harakati za kugombea mpira baada ya kugongana
na wachezaji wa KMC, Uwanja wa Simba Mo Arena ambapo Simba ilishinda mabao 3-1.
Mabao mawili
ya Simba yalifungwa na John Bocco ambaye ni nahodha dakika ya 34 na 75 huku
lile la tatu likifungwa na Ibrahim Ajibu dakika ya 88 na lile la KMC likifungwa
na Charles Ilanfya dakika ya 30.
Meneja wa
Simba, Patrick Rweyemamu amesema kuwa kwa sasa Mkude yupo kwenye uangalizi wa
jopo la madaktari wakimfanyia uchunguzi wa tatizo lake alilolipata kwenye mguu
ukikamilika ripoti yake itatolewa.
"Kwa sasa Mkude yupo chini ya uangalizi wa madaktari ambao wanatazama tatizo lake lipo wapi, uchunguzi ukikamilika ripoti itatolewa," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment