June 19, 2020

MWINYI Kazimoto, nahodha wa Klabu ya JKT Tanzania amesema kuwa ameshamsamehe nyota wa Klabu ya Yanga, Lamine Moro kwa kumchezea mchezo usio wa kiungwana walipokutana Uwanja wa Jamhuri.

Juni 17, Lamine alionekana akimchezea rafu Kazimoto jambo lililosababishwa wote wawili waonyeshwe kadi nyekundu dakika ya 88.

Kazimoto amesema:"Nimezungumza na Lamine kuhusu suala lake na mimi, nimemsamehe kwani masuala ya mipira kuna mambo mengi ila mwisho wa siku maisha lazima yaendelee."

Lamine pia aliomba msamaha kwa mashabiki pamoja na wachezaji wenzake mara baada ya mchezo huo uliokamilika kwa timu zote kugawana pointi mojamoja baada ya kufungana baoa 1-1.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic