RAIS wa awamu ya nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete amesema kuwa mataminio ya mabadiliko ndani ya Yanga ni safari a tatu kufanyika.
Kikwete ameyasema hayo katika hafla ya kutiliana saini ya kuanza safari ya mabadiliko kati ya Yanga, GSM na La Liga ambayo imefanyika jana Hotel ya Serena na kurushwa moja kwa moja kupitia Azam TV na you tube chane ya Yanga.
Kikwete amesema:- "Matamanio ya mabadiliko katika Klabu ya Yanga katika mfumo wa uendeshaji ni ya muda mrefu. Tunakumbuka wakati wa katibu George Mpondela (Castro) alikuja na mapendekezo ya Yanga Kampuni.
"Jaribio kubwa, la pili ni wakati wa mwenyekiti Yusuph Manji alipokuja na dhana ya kukodisha, katika majaribio makubwa hili ni la tatu kwa kumbukumbu zangu, mengine yalikua ya katiba tu"amesema,
Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Mshindo Msolla amesema kuwa baada ya kutiliana saini ya makubaliano ni hatua ya kwanza kuelekea kwenye mabadiliko ambayo ni ndoto ya muda mrefu.
Injinia, Hersi Said Mwakilishi wa GSM amesema kuwa magitaji yao ni kuahca alama na thamani ndani ya Yanga pale watakapoondoka ili iwe kumbukumbu kwa wanachama wajao.
0 COMMENTS:
Post a Comment