June 29, 2020



BAADA ya jana, Juni 28 kulazimisha sare ya bila kufungana na Tanzania Prisons kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Sokoine, leo Simba inarejea Dar es Salaam.

Simba imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara ikiwa na mechi sita mkononi baada ya kufikisha jumla ya pointi 79 ikiwa imecheza mechi 32.

Pointi hizo hazitafikiwa na timu yoyote ndani ya ligi, Yanga ikiwa nafasi ya pili ina pointi 60 ambapo ikishinda mechi zake itafikisha pointi 78 na Azam FC ipo nafasi ya tatu na pointi 59 ikishinda zote itafikisha pointi 77 zote zikiwa zimecheza mechi 32.


Ina mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Azam FC unaotarajiwa kuchezwa Julai Mosi Uwanja wa Taifa hatua ya robo fainali.

Mshindi wa mchezo huo atakutana na mshindi kati ya mchezo wa Yanga na Kagera Sugar.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic