LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa amegundua mbinu mpya ya kuwamaliza wapinzani wake Kagera Sugar ni kuwafunga mabao ya mapema ili kuwajengea wachezaji wake hali ya kujiamini.
Eymael ,kesho Julai 30, atakuwa na kibarua kizito Uwanja wa Taifa, kumenyana na Kagera Sugar iliyo chini ya Mecky Maxime kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho.
Akizungumza na Saleh Jembe, Eymael amesema kuwa anakumbuka alifungwa mabao 3-0 na Kagera Sugar kwenye mchezo wake wa kwanza alipoanza kuinoa Yanga mabaoa 3-0.
“Nilifungwa na Kagera Sugar hilo ninalitambua ila mbinu ambayo nitakuja nayo kwa wakati ujao sio ile ya mwanzo, nimegundua wachezaji wangu wakianza kufunga mapema wanapata hali ya kujiamini hivyo nimewaambia kazi ni moja kupata mabao ya mapema zaidi.
“Tukipata mabao mawili ama matatu kipindi cha kwanza itatuongezea nguvu kupambana na kupata matokeo mazuri, lengo letu tunahitaji kushinda kombe haitawezekana ikiwa tutashindwa kupata matokeo,” amesema Eymael.
Safari ya Yanga ilianza kwa kuitungua mabao 4-0 Iringa United Uwanja wa Uhuru, Desemba 21 mzunguko wa 62, ilishinda 2-0 mbele ya Tanzania Prisons Uwanja wa Taifa, mzunguko wa 32, Januari 26 iliwanyoosha Gwambina kwa bao 1-0 Uwanja wa Uhuru hatua ya 16 bora Februari 26 na kutinga robo fainali.
0 COMMENTS:
Post a Comment