MATTY Longstaff, kiungo anayekipiga ndani ya Klabu ya Newcastle United mwenye umri wa miaka 20 amewekwa kwenye tageti na Klabu ya Udinese Calcio ya Italia.
Kandarasi ya nyota huyo ndani ya Klabu ya Newcastle United inayoshiriki Ligi Kuu England inafika tamati msimu huu jambo linalowapa nguvu Udinese ya Italia inayoshiriki Serie A kuinasa saini yake.
Mbali na Udinese kumuweka kwenye rada inaelezwa kuwa Watford inayoshiriki Ligi Kuu England nayo inahitaji kupata saini ya mchezaji huyo.
Kaka wa mchezaji huyo Sean, amesema ikiwa Newcastle wanahitaji huduma ya mdogo wake ni lazima aongezewe dau la kulipwa kwa wiki tofauti na lile alilokuwa analipwa awali ambalo ni paundi 15,000.
Longstaff ameanza kucheza timu ya wakubwa msimu wa 2019 baada ya kupandishwa kutoka ile ya vijana. Amecheza mechi 7 na kufunga mabao mawili.
0 COMMENTS:
Post a Comment