MECHI ya kirafiki iliyopangwa kuchezwa kesho kati ya Azam FC na KMC huenda ikayeyuka jumla baada ya Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) kuzuia mechi mpaka pale itakapokutana na klabu.
Taarifa ambayo imetolewa na TFF ni kwamba kuanzia sasa hakuna mchezo wowote wa kirafiki utakaoruhusiwa kuchezwa bila ya ruhusa ya TFF.
Taarifa hiyo imeeleza leo TFF inatarajia kukutana na Klabu za Simba, KMC, Azam FC, Yanga na Transit Camp.
Sababu kubwa ni kuchukua tahadhari ya maambukizi ya Virusi vya Corona ambavyo vinaitikisa dunia jambo ambalo lilisababisha masuala mengi ya michezo kusimamishwa ila kwa sasa tayari Serikali imeruhusu masuala ya michezo kuendelea kwa kueleza kuwa hali ya maambukizi imepungua.
Azam FC ilikuwa imepanga kucheza mchezo wa kirafiki na KMC kwa ajili ya kutesti mitambo kabla ya kuendelea na mechi za Ligi Kuu Bara.
Juni 14 Azam FC itakuwa na mchezo wa ligi dhidi ya Mbao FC utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex.
0 COMMENTS:
Post a Comment