June 15, 2020



KIUNGO Fabrice Mugheni, amewaaga rasmi mashabiki wa timu yake ya Rayon Sports ya Rwanda kuwa anaondoka mwishoni mwa msimu huu. 

Fabrice aliwahi kusema kuwa aliombwa video zake na Injinia Hersi Said ambaye ni Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM ambaye pia anahusika na masuala ya usajili ndani ya Yanga.

Kupitia mtandao wake wa Instagram, aliwaaga rasmi mashabiki wa timu hiyo jambo ambalo linatafsiriwa kama huenda akawa alishamalizana na Yanga kwa ajili ya kujiunga na timu hiyo.

Kiungo huyo amesema kuwa ni kweli ataondoka mwishoni mwa msimu huu, ndiyo maana ameamua kuwaaga rasmi mashabiki wa timu yake ili wakiona lolote wasishangae japo hakutaka kuweka wazi ni sehemu gani atakwenda

“Nimeamua kuwaaga mashabiki wa timu yangu ili wakiona chochote wasiwe na maswali mengi ya kujiuliza kichwani, hii inatokana na mimi kuondoka ndani ya Rayon mwishoni mwa msimu huu.

“Haitakuwa rahisi kusema wapi nitaelekea, kwa kuwa nimeaga basi fahamu kuwa nitaondoka mwishoni mwa msimu huu mpaka pale mambo yatakapokuwa kamili watu watafahamu kuwa nimehamia wapi,” alisema mchezaji huyo.

Alipotafutwa Injinia Hersi Said kufunguka juu ya suala la Fabrice Mugheni, alisema: “Kwa sasa kama uongozi unajitahidi kuhakikisha timu inafanya vizuri katika maandalizi ya ligi, hivyo masuala yote ya usajili ukifika muda wake kila kitu kitakuwa wazi.”


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic