June 30, 2020


TIMU ya Namungo FC inayofundishwa na Kocha Mkuu, Hitimana Thiery, leo, Juni 30, imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 mbele ya Alliance FC kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali uliochezwa Uwanja wa Majaliwa, Lindi.

Ushindi huo unaifanya Namungo FC kukata tiketi ys kushirki hatua ya nusu fainali kwenye mchezo w Kombe la Shirikisho ambapo wanamsubiri mshindi wa mchezo kati ya Sahare All Stars atakayemenyana na Ndanda FC, kesho.

Mabao ya Namungo yalipatikana kupitia kwa Bigirimana Blaise dakika ya 40 kwa mkwaju wa penalti baada ya mchezaji wa Alliance kunawa mpira ndani ya 18.

Bao la pili lilipatikana kupitia kwa George Makang'a ambaye alibinuka akiwa ndani ya 18 na kufunga bao matata dakika ya 82 kwa pasi ya Hashim Manyanya.

Ushindi huo unafanya Namungo kushusha presha ya kwanza kwenye hatua ya robo fainali na kuanza kuivutia kasi hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo mikubwa.

Bingwa mtetezi wa taji la Shirikisho kwa sasa ni Azam FC iliyo chini ya Kocha Mkuu, Aristica Cioaba ambaye kesho atamenyana na Simba Uwanja wa Taifa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic