June 1, 2020


BIGIRIMAMA Blaise na Relliants Lusajo ni mitambo ya kucheka na nyavu inaotajwa kuingia anga za Klabu ya Yanga na Simba ambazo zina mpango wa kuboresha vikosi vyao msimu ujao.

Nyota hawa wawili ni mitambo ya kutengeneza mabao ndani ya Namungo FC iliyo chini ya Kocha Mkuu Hitimana Thiery, raia wa Rwanda.

Kwa ujumla wametupia jumla ya mabao 21 kati ya mabao 34, Blaise ametupia mabao 10 na Lusajo ametupia mabao 11 akiwa ni kinara ndani ya klabu hiyo.

Akizungumza na Saleh Jembe, Lusajo amesema kuwa hana tatizo la kucheza timu ya Yanga ama Simba iwapo utaratibu utafuatwa atasaini.


 "Ukiwa mchezaji hauchagui kambi, hivyo ikiwa Yanga ama Simba watahitaji saini yangu sina tatizo nao nitasaini iwapo utaratibu utafuatwa, kikubwa kwangu ni kucheza," amesema.


Blaise amesema kuwa amekuwa akiskia habari hizo ila hajapata taarifa rasmi.

Hassan Bumbuli, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa hawezi kuzungumza kuhusu masuala ya usajili kwa sasa kwani wakati bado ila kinachofanyika ni kuwafuatilia wachezaji wa timu zote.

Patrick Rweyemamu, Meneja wa Simba amesema kuwa muda wa usajili bado haujafika hawezi kuzungumzia masuala hayo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic