June 8, 2020


 MENEJA wa Uwanja wa Fresho Complex, Ombeni Kweka
ambaye ndiye amebuni ramani ya uwanja huo amesema umekamilika kwa asilimia 25 na unatarajiwa kukamilika kwa asilimia 100 kati ya mwaka 2022 na 2023.

Uwanja huo una bustani ya matunda, barabara ya kiwango cha lami, hoteli ya nyota tano, ukumbi wenye uwezo wa kuchukua watu 1,000, eneo la kuogelea (Swimming pool) kwa ajili ya watoto na watu wazima. 

“Uwanja wetu ni bora na wa kisasa, una mandhari nzuri, hakuna wa mfano kwa Kanda ya Ziwa, katika eneo la kuchezea (pitch) kuna mfumo wa mabomba yanayomwagilia maji kutoka chini na mfano hii tunaiona Ulaya.

 "Lakini pia Ujenzi wa majukwaa ukikamilika utakuwa na uwezo wa kubeba watazamaji 18,000 waliokaa na wengine kama 2,000 watakaosimama. 

“Tumeanza kuujenga mwaka 2017 upana wake kwa eneo la kuchezea ni 68 kwa 110, sehemu zingine ambazo hazijakamilika ni eneo la kukimbilia (run away), bwawa la samaki, gym na vyumba vya kubadilishia nguo,” amesema.

4 COMMENTS:

  1. waoh ubunifu wa hali ya juu.Hongera sana Mr.Fresho kwa uwekezaji huu hakika maendeleo yanafanywa na sisi wenyewe watanzania.Mungu amjalie amalize uwanja

    ReplyDelete
  2. Hivyo vipimo vya sehemu ya kuchezea 68 kwa 110 ni uwanja wa mpira wa miguu au!! Maana ni kama hausadifu viwango vya uwanja kamili

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic