PAPY Tshishimbi, nahodha wa Yanga amesema kuwa kikubwa ambacho kinahitajika kwa sasa kutoka kwa mashabiki ni sapoti yao mwanzo mwisho.
Tshishimbi amesema kuwa ni jambo la msingi kwa mashabiki kuendelea kuipa sapoti timu yao kwa kuwa inarejea ikiwa katika ubora wa kipekee.
"Wachezaji licha ya kwamba walikuwa nyumbani bado walikuwa wanafanya mazoezi hivyo kinachotakiwa kwa sasa ni mwendelezo wa sapoti ya mashabiki ambayo ilikuwa ipo tangu zamani.
"Kwa sasa kuna jambo la msingi ambalo tunalifanya ni kuendelea kufanya mazoezi kwa wachezaji waliofiti huku mimi nikiwa naskilizia nirejee kwenye ubora wangu kwani niliumia mazoezini ila ninaendelea vizuri," amesema Tshishimbi.
Jumapili, Yanga itacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya KMC ikiwa ni mchezo wa kupima maendeleo ya wachezaji Uwanja wa Uhuru.
0 COMMENTS:
Post a Comment