July 1, 2020


BRUNO Fernandes, amezidi kutakaka ndani ya kikosi cha Manchester United baada ya jana kutupia mabao mawili mwenyewe kwenye ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Brighton.

Mchezo huo wa Ligi Kuu England ulichezwa bila mashabiki kutokana na kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.

Mabao ya Fernandes yaliokotwa nyavuni dakika ya 29 na 50 huku pazia la kutupia kwa United lilifunguliwa na Mason Greenwood dakika ya 16.

Ushindi huo unaifanya Manchester United inayonolewa na Ole Gunnar Solskjaer kuwa nafasi ya tano ikiwa na pointi 52 huku Brigthon ikiwa nafasi ya 15 na pointi 33 zote zimecheza mechi 32.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic