August 24, 2020

 



AZAM FC inayonolewa na Arstica Cioaba, jana Agosti 23 kwenye kilele cha Azam Festival iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 mbele ya Namungo FC kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Obrey Chirwa alianza kucheka na nyavu dakika ya 37 akimalizia pasi ya Nevere Tigere baada ya mabeki wa Namungo FC na kipa kujichanganya ndani ya 18 kiulaini akauzamisha mpira wavuni.

Steven Sey aliweka mzani sawa dakika 57 kwa kichwa matata akimalizaia pasi ya Edward Manyama.

Bao la ushindi lilipatikana dakika ya 66 kupitia kwa mshambuliaji wa Azam FC, Andrew Simchimba aliyekutana na mpira uliotemwa na kipa wa Namungo FC.


Tamasha hilo lilikuwa ni maalumu kwa ajili ya kutambulisha wachezaji wapya na wale waliokuwa ndani ya kikosi cha Azam FC kwa msimu wa 2019/20 ikiwa ni tayari kwa ajili ya Ligi Kuu Bara inayotarajiwa kuanza Septemba 6.

1 COMMENTS:

  1. Uzi wa Azam kama ulaya jaman Simba mnafeli wapi kutuvalisha sisi Madela

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic