August 10, 2020

SIKU moja baada ya aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba, Senzo Mbatha Mazingiza kutangaza kujiuzulu nafasi yake klabuni hapo kisha kuibukia Yanga, ametakiwa kwenda kukabidhi ofisi ili mambo mengine yaendelee.

 

Senzo raia wa Afrika Kusini, alitangazwa kuwa mtendaji mkuu wa Simba Septemba 7, 2019 akichukua nafasi ya Crescentius Magori na kujiuzulu Agosti 9, 2020, kisha muda mchache akaonekana akiwa na viongozi wa Yanga akisaini nyaraka za mkataba.

 

Inaelezwa kuwa, Senzo ameondoka Simba akiwa hajakabidhi ofisi huku baadhi ya nyaraka muhimu za klabu hiyo zikiwa hazionekani.

 

Kutokana na hali hiyo, aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescentius Magori, alisema: "Hatujui dokumenti zipo wapi mpaka sasa, akumbuke kuwa lazima apate kibali kutoka Simba, kwa namna yoyote ile lazima Yanga waje Simba kwa kuwa hawezi kutumia kibali cha kazi cha kwanza kwa kuwa kinamtambulisha kuwa ni kibali cha Simba.

 

"Vitu vyote muhimu anavyo yeye na alikuwa hapatikani kwenye simu yake ya kawaida, hivyo ninamshauri kiungwana tu leo aende pale Simba akakabidhi vitu vyote, sidhani kama Simba wana tatizo naye, ni maamuzi yake, ninadhani afanye vitu vyote vya utaratibu.

 

"Sio vyote ambavyo amefanya, kuna mambo mengine ya msingi ikiwa ni pamoja na nyaraka dokumenti zetu, gari la Simba alikuwa anendesha, hivyo lazima arejeshe.

 

"Sio lazima awe hapa, ofisi ipo lazima aje, ni muhimu, yeye ni kiongozi, sio mchezaji."

18 COMMENTS:

  1. Si mtoe tangazo kwenye vyombo vya habari "ANATAFUTWA" halafu muweke makosa yake yanayomfanya atafutwe huku mkitoa angalizo ajisalimishe

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nnavyojua mimi nyie nyie mtakuja kwenye huu huu ukurasa na kusema huyu jamaa ni mamluki wa simba time will tell kwani tumeanza kuwajua leo washabiki wa Utopolo furahini hizi siku kadhaa lkn tunajua siku si nyingi moshi utafukuta hapo jangwani mi yangu hayo tu 'mark my word'

      Delete
  2. Kwani kajificha huyo MTU au nae ni morrison

    ReplyDelete
  3. Kwani kajificha huyo MTU au nae ni morrison

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hahahahahahahahahahah!!!!!!! Labda nae anaogopa kupigwa kama alivyokuwa anasema Morrison

      Delete
  4. Hicho kioja,mfa maji haishi kujitapatapa

    ReplyDelete
  5. Magori acha kujiaibisha, wewe ni mtu uliyehudumu kwenye ofis na taasis kubwa; tangu lini Mtendaji Mkuu anatunza Nyaraka?
    Wewe ulipokuwa rumande ulifuatwa kujabidhi "Nyaraka muhimu?"
    Mo karidhia aende kwa kuwa Simba ni kubwa kuliko mtu yeyote, Kaimu Rais Kaduguda kaulizwa kauchuna, wewe unamwita ofisin akukabidhi nini Ofis au zindiko?

    ReplyDelete
    Replies
    1. low thinking capacity hatuwezi kukulaumu

      Delete
    2. If you were a little bit smart to my calibre you would have grasped what I meant but sadly and as usually is the fall back position of the weak is confrontation, insults and the like!

      Delete
  6. labda uelewa. kama alikuwa kiongozi wa juu anapaswa kukabidhi ofisi..kazi kama ya Senzo hawajiuzuru halafu eti wasikabidhi ofisi.
    Nadhani kumchukua Senzo halafu ukashereherea kama vile umemchukua Chama au Kagere au Luis ni kukusea..Sababu Simba ilikuwa bora zaidi ya ambayo ameiongoza Senzo..Akaende aongeze nguvu za Sevilla management

    ReplyDelete
  7. Yaani katoweka na gari pamoja nyaraka muhimu. Huenda huko alpohamia wamenyayuwa mshahara kwa kumuongezea shilingi elfu tatu

    ReplyDelete
  8. Simba na Yanga ninavyoona inapoelekea sasa siyo tena upinzani wa mpira na utani wa jadi bali ni uadui

    ReplyDelete
  9. Simba na Yanga ninavyoona inapoelekea sasa siyo tena upinzani wa mpira na utani wa jadi bali ni uadui

    ReplyDelete
  10. Simba na Yanga ninavyoona inapoelekea sasa siyo tena upinzani wa mpira na utani wa jadi bali ni uadui

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sio upinzani wala uadui wameamua kuwa Comedians(Ze Comedy groups)

      Delete
  11. Senzo kakabidhi nyaraka za klabu la sivyo isomi wako no utopolo chini yamwembe: wanaume tunakutazama unavyotapatapa.

    ReplyDelete
  12. peter c mponeja senzo rudisha nyaraka zetu usituchezee

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic