KLABU ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck leo imetwaa taji lake la tatu ndani ya msimu wa 2019/20.
Simba ilianza na ngao ya jamii, kwa ushindi wa mabao 4-2 mbele ya Azam FC Uwanja wa Taifa ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Patrick Aussems.
Ilianza mechi zake 10 za Ligi Kuu Bara chini ya Aussem kisha ikamlaiza na Sven ambaye alitwaa taji la Ligi Kuu Bara.
Simba ilitwaa taji hilo ikiwa na pointi 79 huku ikiwa na mechi sita mkononi ambazo imezikamilisha na kufanya iwe namba moja na pointi 88 kibindoni.
Leo Agosti 2 imetwaa taji la Kombe la Shirikisho kwa ushindi wa mabao 2-0 mbele ya Namungo FC.
Fainali ya leo iliyoshuhudiwa na mashabiki wengi ndani ya uwanja huo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Habari, Juliana Shonza ambaye alikuwa kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Sven amesema:"Ninafuraha ndani ya moyo kwa kuwa timu imeshinda na tumefikia malengo ambayo tulikuwa tumejiwekea, haikuwa kazi rahisi kufika hapa."
Hongera zao, wakistahili kwa kweli mwaka huu walikuwa bora kuliko wengine wote. Wajiandae kimataifa sasa wasituangushe
ReplyDeleteHongereni sana mabingwa wa nchi mara 3
ReplyDeleteBado kuna maswali?Mshindi wa pili alipigwa 4 ,watatu akapigwa 2 na wanne leo kapigwa 2.Bado kuna maswali?
ReplyDeleteMataji yote msimu huu.Hamna ngebe wala kelele. KIMYAAAAAAAAAAAA.
kweli kabisa tumechapa wote hakuna aliyepona kwa mnyama
DeleteMpira sio tokomile, nadhan wameelewa sasa, wao na sisi tofuti yetu ni kama ardhi na mbingu
ReplyDeleteTutajua mtapoanza kimataifa kama mlikuwa mnachapa kihaga like au ndo kwa mbinu ile ile ya kununua mechi. Tutaona tu ata vitimu vya Burundi vitaanza kuwapa taabu. Au mtaanza kugongwa tano tano. Ndio mtihani wenu. Tutaona tu.
ReplyDeleteMbona unalia-lia au sindano imevunjikia ndani ya mfupa? Utopolo pambaneni na hali zenu.
DeleteKanunue kamba ujinyonge. Sio kwa povu hilo.Kwani nyie Utopolo ile 4G mliuza bei gani?Tatizo lenu ujinga badala ya kujenga timu mmebakia ohh kuna njama.Mmeachwa pointi 16 bado mnaleta visingizio. Ndio maana Luc Aymael aliwatukana
ReplyDeleteLuc aymael katukana na kasema bingwa mpaka uteuliwe hilo vipi
ReplyDeleteUnapigwa 4G bado kweli unalalamika unaonewa? wacha Luc Eyamel awapashe
DeleteKama unaamini kuwa simba kabebwa makombe yote haya matatu basi wewe ni wa kuonea huruma. Hujui mpira ila umejazwa ushabiki
ReplyDelete