UONGOZI wa Yanga umesema kuwa umepeleka mkataba wa kiungo wao, Bernard Morrison kwenye Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) pamoja na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ili waweze kuamua suala la utata wao.
Utata wa mkataba wa Morrison na Yanga umezidi kushika kasi ambapo kila upande unavutia kwao.
Morrison anasema mkataba wake na Yanga ulikuwa ni miezi sita tu na tayari umeisha, huku Yanga wakisema kuwa ana mkataba hadi 2022.
Nyota huyo alijizolea umaarufu kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho wakati Yanga ikishinda mabao 2-0 mbele ya Prisons baada ya kutembea juu ya mpira.
Akizungumza na Spoti Xtra, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela, alisema kuwa suala la Morrison uongozi umelichukulia kwa uzito jambo lililowafanya wapeleke mkataba wa mchezaji huyo CAF na FIFA.
“Tumepeleka mkataba wa Morrison CAF na FIFA, wao wana mamlaka kwenye masuala ya michezo, hatufanyi mambo kwa kubahatisha, hivyo hilo suala lake ninaweza kusema kuwa limekwisha.
"Mashabiki wasiwe na presha tupo sawa na tunajipanga kwa ajili ya msimu ujao mambo yakiwa sawa tutaweka wazi kila kitu," .
TFF imekuaje tena
ReplyDeleteunakata rufaa kabla hukumu
ReplyDeleteTujitulize kwa kuyasghulikia yanayokuja kuliko kupoteza wakati kwa huyu mmoja asiyetambuwa Sheria wala kujijuwa anachokifanya
ReplyDeleteMbona walisema aliposaini waliusajili mkataba TFF na FIFA!? Imekuaje tena waupeleke mkataba mahali ambapo tayari walishakuwa wameusajili?
ReplyDeleteKwani TFF wameshalitolea maamuzi suala hili?
ReplyDeleteMmh kwann wasiachane nae tu na nafasi yake akapewa mtu mwingne anayejitambua
ReplyDeleteTff wote mikia kwa nn wasitoe maamuzi? Wanataka mwisho wa siku wampeleke mikia fc . Viongozi wapo sahihi
ReplyDeletekwani manyani hawana mikia?
DeleteWote sawa!
DeleteHyu mbn mbabaishaji hakuna mandala wake?
ReplyDeleteTff wameshndwa kutoa majbu baada ya kuona yanga hawana mkataba na mchezaji badala yake sshv yanga wameenda fifa,kuwachanganya mashabiki
ReplyDeleteWapeleke na wa Tshishimbi maana waliwadajili wakati mmoja
ReplyDeleteWangeachana naye,,!! Yanga ni kubwa kuliko morison
ReplyDeleteutasajili vipi mkataba mwingine na wa awali haujaisha jamani
ReplyDeletemchezaji anao huo mkataba mpya? au ni awali
ReplyDelete