August 3, 2020


YANGA imedhamiria kufanya kweli ndani ya Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho kwa msimu wa 2020/21 ambapo inaelezwa kuwa inawapigia hesabu wachezaji saba wa kimataifa ambao wanaweza kufiti kikosi cha kwanza.

Miongoni mwa wachezaji hao ni Kiungo, Mukoko Tonombe anayekipiga AS Vita ya DR Congo naye ni raia wa Congo ambaye inaelezwa kuwa huyu wameshafanya naye tayari mazungumzo.

 Eric Rutanga  anayekipiga Rayon Sports, naye anatajwa kumalizana na Yanga muda wowote anaweza kutua sawa na Tuisila Kisanda  wa AS Vita.

 Heritier Makambo yeye ni mshambuliaji naye anatajwa kuingia kwenye rada za Yanga ambapo kuhusu Makambo, Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli alisema kuwa kwa kuwa anatajwa jambo lolote linaweza kutokea kwa sasa anakipiga Horoya AC.

Makambo alicheza ndani ya Yanga msimu wa 2018/19 na alifunga mabao 17 ndani ya ligi. 

Mwingine anayetajwa kuwekwa kwenye rada za Yanga ni Yacouba Songne ambaye ni mchezaji huru pamoja na James Kotei ambaye amewahi kukipiga ndani ya Simba huyu inaelezwa kuwa tayari amemwaga saini ya miaka miwili ndani ya kikosi cha Yanga.

Yidha Sven kiungo anayekipiga ndani ya Kariobarg Sharks ya Kenya pia jina lake linatajwa kuwa kwenye rada za mabingwa hao wa kihistoria.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa hawatafanya makosa kwa msimu ujao kwa kuwa wamedhamiria kufanya usajili makini.

5 COMMENTS:

  1. Kama hawa saba wakisajiliwa, ukijumlisha na wanne wazawa waliokwisha sajiliwa unapata 11. Timu mpya hiyo!

    ReplyDelete
  2. Mmmmmmmh na yule niyonzima wa Rwanda vyukuwap

    ReplyDelete
  3. Mnakosea, mnasajili bila kocha.... Je akija alaf asiwatake hao wakwenu mtafanyeje. Kocha ni hans tu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic