UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa utaendelea kugawa dozi mbele ya wapinzani kwa kuwa wanahitaji kuweka rekodi ndani ya msimu mpya wa 2020/21.
Azam FC imeshinda mechi mbili mfululizo ambazo ni dakika 180 ndani ya uwanja katika mechi za ushindani.
Ilianza mbele ya Polisi Tanzania, Septemba 7 ilishinda bao 1-0, Septemba 11 ilishinda mabao 2-0 mbele ya Coastal Union zote zilichezwa Uwanja wa Azam Complex.
Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa mpango wao ni kuendelea kufanya vizuri kwenye mechi zote.
"Kuanza kwetu vizuri ni furaha kwetu na mpango wetu ni kuona kwamba tunaweza kuendeleza rekodi ya kupata ushindi kwenye mechi zetu zote zinazokuja," amesema.
Mchezo ujao wa Azam FC ni dhidi ya Mbeya City, Septemba 20 Uwanja wa Sokoine.
Mmechezea chamanzi mmeanza mdomo kafanyeni Na hivyo mikoani Kama mnadhani rahisi.
ReplyDeleteHeeheee kila mwaka wanaanza ligi kwa vishindo lkn ligi kabla ya kuingia mzunguko wa pili wanambwela.
Delete