September 15, 2020



SENZO Mbatha, mshauri mkuu ndani ya Klabu ya Yanga kuelekea kwenye mfumo wa mabadiliko amesema kuwa anafurahia maisha yake ya sasa ndani ya timu hiyo kutokana na sapoti anayopata.

Mbatha aliibukia ndani ya Yanga akitokea Klabu ya Simba muda mfupi baada ya kutangaza kujiuzulu nafasi yake ambapo alikuwa ni bosi ndani ya Simba akiwa ni Mtendaji Mkuu,(C.E.O).

Mbatha amesema:-"Ninaheshimu kuhusu Yanga kwa kuwa ina namba kubwa ya mashabiki, namba kubwa ya wadhamini ambao wapo ndani yake ikiwa ni pamoja na Kampuni ya GSM, wadhamini wetu SportPesa.

"Ninafurahia kufanya kazi na mwenyekiti Msolla,(Mshindo) sapoti ambayo tunapata inatupa matokeo mazuri ya kile ambacho tunakihitaji hasa kwa sasa tukiwa kwenye aina ya mpira wa kisasa.

"Mpira wa kisasa unahitaji kila kitu kuwa bora kuanzia sehemu ya kuchezea sehemu ya mazoezi, miundombinu pamoja na ushirikiano jambo ambalo linatupa nguvu.

"Katika kila jambo tunajiandaa kwa utayari ili kuweza kuleta ushindani ndani na nje ya uwanja," amesema.

Akiwa kiongozi ndani ya Yanga, ameshuhudia timu yake ikicheza mechi mbili za Ligi Kuu Bara ambapo ilikuwa ni mbele ya Tanzania Prisons kwenye sare ya kufungana bao 1-1 na mchezo wa pili ilikuwa mbele ya Mbeya City, ilishinda bao 1-0 zote zilichezwa Uwanja wa Mkapa.

13 COMMENTS:

  1. Mwandishi lugha ya Kiswahili ni tajiri sana wa maneno sahihi ya kutumia. Hivi kumbe Senzo bado ni bosi wa Simba au alikuwa bosi wa SImba? Kama bado ni bosi huko sasa huku Yanga anafanya nini? Usituchonganishe!!!!!!

    ReplyDelete
  2. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Soma kichwa cha habari halafu ujitathimini kabla hujakomenti alichoandika mwenzako."Bosi wa Simba......." Kwani Senzo bado ni bosi wa Simba? Hiyo ndiyo matiki ya aliyekomenti

      Delete
  3. Asiyejua kusoma anaweza kufika hapa tulipo kweli??try to think before putting your coments on blog,inawezekana wewe ndio hujaelewa mantik ya jamaa aliyekoment hapo juu,SENZO ALISHAONDOKA SIMBA NA TAYARI NI MUAJIRIWA YANGA,SASA IWEJE MWANDISHI ANAENDELEA KUMTAJA SENZO KAMA BADO NI MTUMISHI WA SIMBA?KWANINI ASITUMIE CHEO WALICHOMPATIA YANGA?ELEWA BROTHER NA POVU RUKSAAA.

    ReplyDelete
  4. Bora wizara ya habari imeamua kufuatilia wandishi makanjanja ambao ni wenye vyeti visivyo kidhi kuwa mwandishi kisheria.Bosi wa Simba anafurahia maisha Yanga? Hatukelewi maana Senzo alishaondoka Simba.Naamini uandishi ni lugha hivyo unapaswa kutumia kalamu yako kwa umakini na kuzingatia maadili ya uandishi kama kweli ulienda school of journalism.

    ReplyDelete
  5. Jamani poleni sana. Kila siku mnaandika juu ya matumizi sahihi ya kuandika. Hapa siyo uandishi hata lugha fasaha haipo.Kama mwandishi alitaka kuipamba habari yake ili ipate "attention Gette", angesema "Bosi wa Zamani wa Simba afurahia maisha mapya", hiyo ingetosha na msomaji angeingia ndani kumjua nani na anafurahia nini na wapi.

    ReplyDelete
  6. Mwandishi jitathimini na uandishi wako.Imeshindikana vipi kuandika Bosi SENZO afungukia maisha yake Yanga? Tunavyoelewa Senzo alishaondoka klabu ya Simba na sio mmoja wa mabosi wa Simba.

    ReplyDelete
  7. Niwasaidie huyu hajakosea ila anaipa Simba sifa ionekane ndiyo walimleta Senzo.Heading inamtaja hivyo lkn maelezo ndani ni Yanga .Hiyo inahitaji uelewa .Tatizo wengi mlikimbia shule lugha nyingine zikitumika kuwaelimisha hamtaelewa mfano (maudhui)nk ktk utoaji wa taarifa inazingatiwa,na haya yapo primary,olevel
    Sasa wenzangu na mie maadamu unajua kusoma na kuandika na una smart phone na mkono wa mjinga uandike popote unakurupuka kumtukana kama siyo kumfundisha ,japo kuwa naye aache Usimba.Japo inawezekana hata kibari Cha kufanya kazi bado ni cha Simba

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umekula maharage ya wapi wewe?????umeandika nini hapo?

      Delete
  8. Pole kwa kujikwaa.Sikujua kuwa wenzangu mmeliona ili pia. Ata neno afungukia linagoma kuendana na habari yenyewe. Ata kama ni kuwavuta wasomaje wengine lakini naona lugha imegoma.

    ReplyDelete
  9. Waandishi wengi tulionao sasa wanapoteza ladha ya uandishi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic