HII ni rekodi mpya ya Yanga ambayo imejirudia baada ya kupita takribani misimu kumi ndani ya Ligi Kuu Bara.
Yanga ambayo ilianzishwa mwaka 1935, ndiyo mabingwa wa kihistoria wa
Ligi Kuu Bara baada ya kulitwaa mara 27, wakifuatiwa na Simba wenye mataji 21.
Wikiendi iliyopita ambapo Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21 ilianza,
ndiyo Yanga iliweka rekodi hiyo baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Prisons
kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.
Rekodi ambayo Yanga imeiweka ni ya kushindwa kuibuka na ushindi katika
mechi ya kwanza ya ligi kwa msimu wa pili mfululizo. Awali iliwahi kufanya
hivyo katika msimu wa 2011/12 na 2012/13. Kisha haijawahi kujirudia hadi msimu
huu.
Ikumbukwe kuwa, msimu uliopita, Yanga ilianza kwa kupokea kichapo
kutoka kwa Ruvu Shooting cha bao 1-0, msimu huu ikatoka sare ya 1-1 na
Priosons.
Katika msimu wa 2011/12, Yanga ikiwa nyumbani, ilianza ligi kwa
kufungwa Yanga 0-1 JKT Ruvu ambayo kwa sasa ni JKT Tanzania, kisha 2012/13
ikatoka 0-0 na Prisons ugenini.
Msimu wa 2019/20, Yanga ilifungwa na Ruvu Shooting bao 1-0, kisha
msimu huu ikatoka sare ya 1-1 na Prisons. Mechi hizo zote Yanga ilikuwa
nyumbani.
Wakati Yanga ikianza msimu wa 2011/12 kwa kipigo, ilimaliza ligi
nafasi ya tatu ikikusanya pointi 49. Mabingwa walikuwa Simba waliokusanya pointi
62, nafasi ya pili ilishikwa na Azam iliyokuwa na pointi 56.
Msimu wa 2012/13, Yanga licha ya kuanza kwa sare, lakini ilikuwa
bingwa kwa kukusanya pointi 60. Nafasi ya pili ilishikwa na Azam iliyokuwa na
pointi 54 na Simba ya tatu ikiwa na pointi 45.
2019/20, Yanga ilipofungwa mechi ya kwanza, ilimaliza ligi nafasi ya
pili ikiwa na pointi 72 katika nafasi ya pili nyuma ya mabingwa Simba
waliokusanya pointi 88.
Msimu huu imeanza kwa sare, kitakachotokea mwisho wa msimu kila mmoja
anakisubiri kama kitajirudia kile kilichotokea msimu wa 2012/13.
Ukiangalia katika rekodi hizo, Yanga ilicheza na timu zote za majeshi
ambazo ni JKT Tanzania, Ruvu Shooting na Prisons mara mbili.
KOCHA ZLATKO
ASHANGAA
Baada ya
kuanza ligi kwa sare, mashabiki wa timu hiyo walianza kutoa maneno mengi juu ya
kikosi chao hicho ambapo Kocha wa Yanga, Zltako Krmpotic, aliwashangaa akisema:
“Hakuna tatizo lolote juu ya kuanza vibaya kwenye ligi kwani hali hiyo inaweza
kuitokea timu yoyote ile. Tulicheza vizuri sana lakini mwisho tukapata matokeo
hayo ambayo ni kawaida sana.
“Cha muhimu
zaidi ni kwamba kwenye mechi ijayo tutaongeza umakini kuhakikisha tunapata
matokeo mazuri.”
MSIMU: 2011/12
MATOKEO: Yanga 0-1 JKT Ruvu
NAFASI: 03
POINTI: 49
MSIMU: 2012/13
MATOKEO: Prisons 0-0 Yanga
NAFASI: 01
POINTI: 60
MSIMU: 2013/14
MATOKEO: Yanga 5-1 Ashanti
NAFASI: 02
POINTI: 56
MSIMU: 2014/15
MATOKEO: Mtibwa 2-0 Yanga
NAFASI: 01
POINTI: 55
MSIMU: 2015/16
MATOKEO: Yanga 2-0 Coastal
NAFASI: 01
POINTI: 73
MSIMU: 2016/17
MATOKEO: Yanga 3-0 African Lyon
NAFASI: 01
POINTI: 68
MSIMU: 2017/18
MATOKEO: Yanga 1-1 Lipuli
NAFASI: 03
POINTI: 52
MSIMU: 2018/19
MATOKEO: Yanga 2-1 Mtibwa
NAFASI: 02
POINTI: 86
MSIMU: 2019/20
MATOKEO: Yanga 0-1 Ruvu
NAFASI: 02
POINTI: 72
MSIMU: 2020/21
MATOKEO: Yanga 1-1 Prisons
NAFASI: ???
POINTI: ???
0 COMMENTS:
Post a Comment