September 10, 2020

 


MZUNGUKO wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu wa 2020/21 umekamilika kwa timu 9 kupambania pointi tatu huku wachezaji wakipambana kuweka rekodi mpya.

Kwenye mechi 9 zilizochezwa yamefungwa jumla ya mabao 14 huku watupiaji wote wa kigeni na wazawa ikiwa ni pamoja na Obrey Chirwa anayekipiga ndani ya Azam FC na Michael Sarpong anayekipiga ndani ya Yanga wakishindwa kuvunja rekodi iliyowekwa na Kagere kwa muda wa misimu miwili mfululizo.

Kagere ndani ya misimu miwili ametupia mabao 45,msimu wake wa kwanza wa 2018/19 alitupia mabao 23 alianza kuwatungua Tanzania Prisons dakika ya kwanza ikiwa ni bao la mapema zaidi kwa pasi ya John Bocco na msimu wa pili alianza kupachika bao la kwanza dakika ya kwanza, wakati Simba ikishinda mabao 3-1 mbele ya JKT Tanzania, Uwanja wa Uhuru kwa pasi ya Mzamiru Yassin.

Kwa msimu huu wa 2020/21, Kagere alianzia benchi mchezo wake wa kwanza mbele ya Ihefu na kushuhudia bao la kwanza kwa Simba likifungwa na John Bocco dakika ya 10 huku lile la mapema zaidi likifungwa na Lambart Charlse dakika ya 7 yeye anakipiga Tanzania Prisons ilikuwa mbele ya Yanga, Uwanja wa Mkapa.

Wengine ambao walicheka na nyavu ikiwa ni pamoja na Michael Sarpong wa Yanga yeye alipachika bao dakika ya 19 na Obrey Chirwa wa Azam FC alipachika bao la kwanza dakika ya 44.

Rekodi nyingine ya Kagere ambayo imeshindikana kuvunjwa kwa msimu huu kwenye mechi za mwanzo ni kwa wachezaji kushindwa kufunga mabao zaidi ya mawili, tofauti na msimu uliopita ambapo ni nyota wawili waliweka rekodi hiyo ambao ni Lukas Kikoti wa Namungo na Kagere.

8 COMMENTS:

  1. Duh hizo rekodi zenu pasua kichwa...ukisoma huelewi ama huoni tija ya makala kabisa!!!

    ReplyDelete
  2. Tafuta vitu vya msingi siyo kutuandikia upuuzi huu.

    ReplyDelete
  3. Mwandishi wanaonyesha mahaba yake kiuandishi kwa kupendelea Simba....hii ni shida

    ReplyDelete
  4. Yaan habar nmeieudia mara tatu hata siielewi

    ReplyDelete
  5. Acha kuandika kama mtu wa darasa la nne..Sarpong amekwama vipi wakati ndiyo kwanza hata ajacheza mechi mbili za ligi?hizo ni takwimu za akili yako hivyo basi ni bora ukazificha kwenye kona ya ubongo wako...ambapi zinastahili kuwa..usiwe unatiandikia upuuzi ambao unajisikia...kicha cha habari ndiyo kitashauri mtu kusoma habara...sasa kama kichwa ni takataka inaonyesha hata ndani ya habari ni uozo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Record iliyokusudiwa hapo ni ya kupachika bao Dk ya kwanza ktka game za ufunguzi.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic